انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٦

قُلِ ٱدْعُوا۟ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِۦ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ ٱلضُّرِّ عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا ٥٦

{56} Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema, "Sema" kuwaambia wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, ambao walifanya wenza badala yake, wakawaabudu kama wanavyomuabudu Mwenyezi Mungu, na wanawaomba kama wanavyomuomba, huku akiwalazimisha kusahihisha wanayodai hayo, na waliyoyaitakidi ikiwa ni wakweli, "Waombeni hao mnaowadai" kuwa ni miungu badala yake Yeye, basi angalieni watawanufaisha au wanaweza kuwazuilia madhara yoyote? Hao, "Hawawezi kuwaondolea madhara" kama vile magonjwa, ufukara, ugumu na mfano wake. Hawawezi kuyazuia kabisa, wala hawana uwezo wa kuhamisha kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine, au kutoka kwa ugumu moja hadi kwa kilicho kidogo zaidi yake. Basi ikiwa hii ndiyo sifa yao, kwa nini mnawaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Kwani wao hawana ukamilifu wala kitendo chenye manufaa. Basi kuwafanya miungu ni upungufu katika dini na akili na ni upumbavu katika rai. Na katika yanayoshangaza ni kwamba upumbavu unapokuwa ndiyo ada, na ukazoewa, na ukachukuliwa kutoka kwa akina baba wapotovu, huonwa na mwenye kuwa na rai iliyo sawasawa na akili yenye manufaa, na anaona kuwa mumfanyie dini Mwenyezi Mungu tu, ambaye ni Mmoja tu, wa pekee, Mkamilifu, Mneemeshaji kwa neema zote za dhahiri na zilizofichikana kwamba ni upumbavu na jambo la kustaajabisha, kama walivyosema washirikina, "Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu."