الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا تَقْرَبُوا۟ ٱلزِّنَىٰٓ ۖ إِنَّهُۥ كَانَ فَـٰحِشَةً وَسَآءَ سَبِيلًا ٣٢
{32} Na kukataza kuikaribia zina kuna maana kubwa zaidi kuliko kukataza kuifanya tu, kwa sababu hilo linajumisha kukatazwa kwa matangulizi yake yote na sababu zake. Kwa maana, yeyote mwenye kuzunguka karibu na himaya, anakaribia kuanguka ndani yake, hasa jambo hili, ambalo ndani ya nafsi nyingi kuna sababu za nguvu za kuliitia. Na Mwenyezi Mungu aliuelezea uzinzi na ubaya wake kwamba ni, "uchafu." Yaani, dhambi inayojulikana uchafu wake katika sheria, na akili, na maumbile ya asili, kwa sababu unajumuisha kuthubutu kufanya maharamisho yanayohusiana na Mwenyezi Mungu, na mwanamke, na familia yake au mumewe, kuharibu malazi yao, na kuchanganya nasaba, na uharibifu mwingine. Na kauli yake, "na njia mbaya" yaani, njia mbaya zaidi ni njia ya mwenye kuthubutu kutenda dhambi hili kubwa.