الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ وَجَعَلْنَـٰهُ هُدًى لِّبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُوا۟ مِن دُونِى وَكِيلًا ٢
{2} Yeye Muumba mara nyingi huunganisha kati ya unabii wa Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na unabii wa Musa - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na vitabu vyao na sheria zao; kwa sababu vitabu vyao ndivyo vitabu bora zaidi, na sheria zao ndizo sheria kamili zaidi, na unabii wao ndio unabii wa hali ya juu zaidi, na wafuasi wao ndio waumini wengi zaidi. Na ndiyo sababu akasema hapa, "Na tulimpa Musa Kitabu" ambacho ni Taurati. "Na tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili" ili waongoke kwacho katika giza la ujinga hadi katika kuijua haki. "Kwamba msimfanye yeyote asiyekuwa mimi kuwa mwakilishi wenu." Yaani, tuliwaambia hayo, na tukawateremshia Kitabu kwa ajili ya hilo, ili wamwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na wamrudie, na wamfanye yeye peke yake kuwa ndiye mtegemewa wao, mwenye kuendesha mambo yao ya kidini na ya kidunia, na wala wasijifungamanishe na yeyote asiyekuwa yeye miongoni mwa viumbe ambao hawamiliki kitu na wala hawawafai kwa chochote.