الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَجَعَلْنَا ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ ءَايَتَيْنِ ۖ فَمَحَوْنَآ ءَايَةَ ٱلَّيْلِ وَجَعَلْنَآ ءَايَةَ ٱلنَّهَارِ مُبْصِرَةً لِّتَبْتَغُوا۟ فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ وَلِتَعْلَمُوا۟ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلْحِسَابَ ۚ وَكُلَّ شَىْءٍ فَصَّلْنَـٰهُ تَفْصِيلًا ١٢
{12} Anasema Yeye Mtukufu, "Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili" yenye kuashiria ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu na upana wa rehema yake, na kwamba Yeye tu ndiye anayestahiki kuabudiwa. "Tena tukaifuta ishara ya usiku;" yaani, tukaifanya kuwa na giza ili mtulie humo na mpate starehe. "Na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza, ili mtafute fadhila itokayo kwa Mola wenu Mlezi" katika maisha yenu, na shughuli zenu, na biashara zenu, na safari zenu, "na ili mpate kujua" kwa kufuatana usiku na mchana, na kutofautiana kwa mwezi, "idadi ya miaka na hesabu" ili mpate kujenga juu yake chochote mnachotaka katika masilahi yenu. "Na kila kitu tumekifafanua kwa kina waziwazi." Yaani, tumezibainisha ishara na kuzibadilishabadilisha ili mambo yaweze kupambanuka, na haki ibainike kutoka kwa batili, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote."