النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
مَنْ عَمِلَ صَـٰلِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ٩٧
{97} Basi ndiyo sababu, akataja malipo ya watendaji katika dunia na Akhera. Akasema, "Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini" kwa maana Imani ni sharti la matendo mema kuwa sahihi na kukubaliwa. Bali hayaitwi matendo mema isipokuwa kwa imani. Na pia imani inahitaji kutenda mema. Kwani, imani ni usadikisho thabiti wenye kuzaa matendo ya viungo ya wajibu na yapendekezwayo. Kwa hivyo mwenye kujumuisha kati ya imani na matendo mema, "hakika tutamhuisha uhai mwema" kwa kuufanya moyo wake kutua na kutulia kwa nafsi na kutoangalia yenye kuushawishi moyo wake na Mwenyezi Mungu atampa riziki nzuri halali kutoka asikotarajia, "na hakika tutawapa" katika Akhera, "ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda" miongoni mwa aina mbalimbali za starehe ambazo hakuna jicho lililowahi kuyaona, wala hakuna sikio lililowahi kuyasikia wala hayajawahi kupitia katika moyo wa binaadamu yeyote. Basi Mwenyezi Mungu atampa mazuri duniani na Akhera pia.