النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَوْمَ نَبْعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا ثُمَّ لَا يُؤْذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ ٨٤ وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ٱلْعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ٨٥
{84-85} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya hali ya hawa ambao walikufuru katika Siku ya Qiyama, na kwamba hawatakubaliwa udhuru wowote wala hawataondolewa adhabu, na kwamba washirikishwa wao hao watawakataa, na watakiri wenyewe kwamba walikuwa makafiri na kwamba walimsingizia Mwenyezi Mungu. Alisema Yeye Mtukufu, "Na siku tutakapomtoa shahidi kutoka katika kila umma" ili ashuhudie juu yao matendo yao na kile walichomjibu kwacho mlinganiaji aliyekuwa analingania kwenye wongofu. Na shahidi huyu ambaye Mwenyezi Mungu atamtoa kwao atakuwa ndiye shahidi msafi zaidi na mwadilifu wao zaidi, na wao ni Mitume, ambao, watakaposhuhudia, basi itatimia hukumu juu yao. "Kisha hawataruhusiwa wale waliokufuru" ili waweke udhuru wao. Kwa maana kuweka kwao udhuru baada ya wao kwisha jua kwa yakini ubatili wa wayafanyayo ni udhuru muongo usioweza kuwasaidia kitu. Na pia wakiomba kurudi duaniani ili watekeleze ambayo hawakutekeleza vyema, hawajibiwi wala hawaridhiwi. Bali wanaanzishiwa adhabu kali ambayo hawatahafifishiwa, wala kupewa muhula kuanzia wanapoiona, kwa sababu hawana mazuri yoyote. Na matendo yao yatahesabiwa tu, na kudhibitiwa, na watafanywa kuyaungama, na watafedheheshwa.