انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨١

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَـٰلًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلْجِبَالِ أَكْنَـٰنًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلْحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ ٨١

{81} "Na Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba;" yaani, katika viumbe vyake ambavyo hamkuvitengeneza nyinyi, "vivuli" kama vile vivuli vya miti, milima, vilima, na mfano wake. "Na amewafanyia maskani milimani;" yaani, mapango yenye kuwahifadhi kutokana na joto, baridi, mvua, na maadui. "Na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto." Na Mwenyezi Mungu hakutaja baridi, kwa sababu ilitangulia kwamba mwanzoni mwa sura hii zimetajwa neema za kimsingi, na mwishoni mwake zimetajwa neema kamilishi na timilizi. Na kuzuia kutokana na baridi ni katika neema za kimsingi, na tayari alikwisha itaja mwanzoni mwa sura hii katika kauli yake, "katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo" na "nguo za kuwakinga katika vita vyenu" kama vile deraya za kawaida na deraya za vifungo, na mfano wake. "Ndivyo hivyo anawatimizia neema zake" ambapo aliwapa kwa wingi katika neema zake zisizowezekana kuhesabika "ili" mnapozikumbuka neema za Mwenyezi Mungu na kuziona zimewafunika katika kila njia, "mtapata kujisalimisha kwake." Kwa sababu ya ukuu wake, na mfuate amri yake, na kuzitumia katika kumtii yule aliyewapa kuzisimamia. Kwa hivyo wingi wa neema ni katika sababu zinazowafanya waja kuzidisha shukrani na kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake.