النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ ظَالِمِىٓ أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا۟ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوٓءٍۭ ۚ بَلَىٰٓ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ٢٨
{28} Kisha akataja kile atakachowafanyia wakati wa kifo na katika Siku ya Qiyama, akasema, "Wale ambao Malaika huwafisha huku wamejidhulumu!" Yaani, wanawafisha katika hali hii ambayo udhalimu wao na upotovu wao umekithiri, na tayari ilikwisha julikana aina za adhabu, aibu, fedheha na kudunishwa ambavyo watapata katika mahali hapo. "Basi wanasalimu amri" na kukataa vile walivyokuwa wakiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, na watasema, "Hatukuwa tukifanya ubaya wowote" Lakini wataambiwa, "Hasha!" Mlikuwa mkifanya ubaya. "Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyokuwa mkiyatenda." Basi kukataa kwenu huku hakutawanufaisha kwa chochote. Hili ni katika baadhi ya hali katika Siku ya Qiyama. Watayakataa yale waliyokuwa wakifanya katika dunia, wakidhani kwamba hilo litawafaidi. Lakini vitakaposhushudia dhidi yao viungo vyao na yakawa wazi yale waliyokuwa wakifanya, watakiri na kukubali, na ndiyo maana, hawataingia Motoni mpaka watakapokiri dhambi zao.