النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِ ۚ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِى ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ ١٢٧ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوا۟ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ ١٢٨
{127 - 128} Kisha akamuamrisha Mtume wake kuwa na subira katika kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu na kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu katika hilo na wala asijitegemee nafsi yake. Akasema, "Na subiri, na subira yako iko kwa Mwenyezi Mungu tu." Yeye ndiye anayewanusuru humo na kuwaweka imara. "Wala usiwahuzunikie" ukiwaita na hukuwaona wakikubali mwaliko wako; huzuni haikusaidii chochote. "Wala msiwe katika dhiki." Yaani, dhiki na aibu "kutokana na hila zao" kwani vitimbi vyao vinawarudia, na wewe ni miongoni mwa wachamungu na wafanyao wema, na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamungu na wafanyao wema, kwa nusura yake, na kufaulu, na uwongofu. Na hao ndio walioogopa ukafiri na dhambi, na wakatenda mema katika kumwabudu Mwenyezi Mungu. Kwamba walimwabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba wanamwona; ikiwa hawamuoni, basi anawaona, na ihsani kwa viumbe ni kwa kuwanufaisha wao kwa kila njia. Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie tuwe miongoni mwa watu wema na wafanyao wema.
Imekamilika tafsiri ya Surat An-Nahl. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.