النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا فُتِنُوا۟ ثُمَّ جَـٰهَدُوا۟ وَصَبَرُوٓا۟ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ ١١٠
{110} Yaani, kisha "Mola wako Mlezi" ambaye aliwalea waja wake wamkusudiaye yeye tu kwa upole wake na wema wake "ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu;" kwa wale waliohama katika njia yake, na akayaacha makazi yake, na mali zake akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu, na akajaribiwa kwa sababu ya dini yake ili arudi katika ukafiri, lakini akawa imara juu ya imani yake, na akawa na yakini iliyo safi zaidi, kisha akapambana na maadui wa Mwenyezi Mungu ili awaingize katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa ulimi wake na mkono, na akasubiri juu ya ibada hizi ngumu kwa wengi wa watu. Basi hizi ndizo sababu kubwa zaidi za kupata kwazo kipawa kikubwa na tunu bora zaidi, ambazo ni msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa madhambi, madogo yake na makubwa yake, ambazo zinajumuisha kuondoka kwa kila kitu kinachochukiwa, na pia kupata rehema yake kubwa, ambayo kwayo zilitengenea hali zao, na mambo ya dini yao na dunia yao yakanyooka, basi wana rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyama.