ابراهيم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِيمُ رَبِّ ٱجْعَلْ هَـٰذَا ٱلْبَلَدَ ءَامِنًا وَٱجْنُبْنِى وَبَنِىَّ أَن نَّعْبُدَ ٱلْأَصْنَامَ ٣٥
{35} Yaani, "na" mtaje Ibrahim -rehema na amani ziwe juu yake - katika hali hii nzuri. "Na Ibrahim aliposema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ujaalie mji huu" mtakatifu "uwe wa amani." Basi Mwenyezi Mungu akamuitikia dua yake kisheria na kimajaliwa. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akauharamisha katika sheria, na akaweka sababu za kuuharamisha kimajaliwa kama inavyojulikana, kiasi kwamba hakuna hata dhalimu mmoja aliyeutakia ubaya isipokuwa Mwenyezi Mungu alimuangamiza. Kama alivyowafanyia watu wa tembo na wengineo. Na alipouombea amani, aliuombea huo na watoto wake amani. Akasema "uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu." Yaani, niweke kando mimi na wao na kuiabudu na kuifahamu.