انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ابراهيم
السورة ١٤

ابراهيم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣

ٱلَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا عَلَى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ فِى ضَلَـٰلٍۭ بَعِيدٍ ٣

{3} Kisha akawaeleza kuwa wao ndio wale wanaopendelea "uhai wa dunia hii kuliko Akhera" wakauridhia, na wakatulia, na wakaisahau nyumba ya Akhera. "Na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu" aliyowawekea waja wake, na akaibainisha katika Vitabu vyake na juu ya ndimi za Mitume wake. Basi watu hawa walimkataa Mola wao kwa ukaidi na vita. "Na wanaitakia" Njia hiyo ya mwenyezi Mungu "ijipinde;" yaani, wanafanya bidii katika kuichanganya na kuifanya kuwa mbovu ili kuwatenga watu nayo, lakini Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa kuikamilisha nuru yake, hata kama makafiri wataichukia. "Hao' waliotajwa maelezo yao “wako katika upotevu wa mbali” kwa sababu wao wenyewe walipotea, na wakawapoteza wengine, na wakampinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakapigana vita nao. Basi ni upotofu gani ulio mbali zaidi kuliko huu? Na ama watu wa imani, wao wako kinyume na hawa. Wao wanamuamini Mwenyezi Mungu na ishara zake, na wanapendelea akhera kuliko dunia, na wanalingania katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaifanya kuwa nzuri namna wawezavyo, na wanabainisha unyoofu wake.