ابراهيم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ بَدَّلُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا۟ قَوْمَهُمْ دَارَ ٱلْبَوَارِ ٢٨
{28} Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu, akieleza hali ya wale waliomkadhibisha Mtume wake miongoni mwa makafiri wa Kiquraishi na namna hali yao ilivyoisha: "Je hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru." Na neema ya Mwenyezi Mungu ni kumtuma Muhammad - Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - kwao akiwalingania kufikia heri katika dunia na akhera na kuokoka na maovu ya dunia na Akhera. Basi wakaibadilisha neema hii kwa kuikataa na kuikufuru, na kuzuia dhidi yake wao wenyewe, na kuwazuia wengine dhidi yake, mpaka "wakawafikisha kaumu yao kwenye nyumba ya maangamizo?" Yaani, Moto. Kwa maana walikuwa ndiyo sababu ya kupotea kwao, na wakawa ni balaa kwa kaumu yao kwa kuwa ilidhaniwa kuwa ni wenye manufaa. Na katika hayo ni kwamba waliwapambia kwamba watoke katika siku ya Badr kupigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa hivyo yakawapata yaliyowapata. Na wengi katika wakuu wao na viongozi wao wakauawa katika tukio hilo.