ابراهيم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَبَرَزُوا۟ لِلَّهِ جَمِيعًا فَقَالَ ٱلضُّعَفَـٰٓؤُا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوٓا۟ إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا مِنْ عَذَابِ ٱللَّهِ مِن شَىْءٍ ۚ قَالُوا۟ لَوْ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ لَهَدَيْنَـٰكُمْ ۖ سَوَآءٌ عَلَيْنَآ أَجَزِعْنَآ أَمْ صَبَرْنَا مَا لَنَا مِن مَّحِيصٍ ٢١
{21} "Na wote;" yaani, viumbe "mbele ya Mwenyezi Mungu" itakapopulizwa katika barugumu, kisha wakatoka makaburini kwenda kwa Mola wao Mlezi, na watasimama katika ardhi iliyotandazwa, tambarare, uwanda. Hutaona humo mdidimio wala muinuko. Na watajitokeza mbele yake wala hakitafichika kwake chochote cha kufichika kutoka kwao. Kisha wataanza kubishana huku kila mmoja akijitetea nafsi yake kiasi awezavyo, lakini watawezaje kufanya hivyo? Basi watasema "wanyonge;" yaani, wafuasi waliokuwa wakiiga "watawaambia wale waliotakabari" yaani wale waliofuata ambao wao ndio viongozi katika upotovu; "Hakika sisi tulikuwa wafwasi wenu." Yaani, katika dunia mlipotuamrisha upotevu, na mkatupambia upotevu huo basi mkatupoteza. "Basi hebu hamtuondolei kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu?" Hata kama ni cha uzito wa chembe "watasema" hao waliofuatwa, na viongozi, "Tuliwapoteza kama tulivyopotea, basi "Lau Mwenyezi Mungu angelituongoa, basi hapana shaka nasi tungeliwaongoza" kwa hivyo hakuna mtu yeyote atakayemfaa mwingine. "Ni mamoja kwetu tukipapatika" kutokana na adhabu "au tukisubiri: juu yake. "Hatuna pa kukimbilia popote" kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu.