انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ابراهيم
السورة ١٤

ابراهيم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٠

قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِى ٱللَّهِ شَكٌّ فَاطِرِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ قَالُوٓا۟ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا تُرِيدُونَ أَن تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ ءَابَآؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ ١٠

10. Lakini walidanganya katika hayo, na wakadhulumu, na ndiyo maana "wakawaambia Mitume wao: Je, kuna shaka kuhusiana na Mwenyezi Mungu" kwa sababu yeye ndiye wa dhahiri zaidi ya vitu vyote na wa wazi zaidi. Kwa hivyo mwenye kuwa na shaka juu ya Mwenyezi Mungu "Muumba wa mbingu na ardhi" ambaye uwepo wa vitu vyote unategemea juu ya uwepo wake, basi huyo hana imani yoyote katika habari zozote, hata mambo yanayohisika. Na ndiyo maana Mitume hao wakawazungumzisha kwa mazungumzo ya mtu ambaye hana shaka naye, na wala haipasi kuwepo na shaka kuhusiana naye. "Yeye anawaita" katika manufaa yenu na masilahi yenu, "ili awafutie katika madhambi yenu, na awaache mpaka muda uliowekwa." Yaani, ili awalipe kwa sababu ya kuitikia wito wake kwa malipo ya haraka na ya baadaye. Na wala hakuwaita ili anufaike na ibada yenu, bali manufaa yake yatarudi kwenu. Lakini wao wakawajibu Mitume wao kama wanavyofanya wapumbavu wajinga, "na wakasema" wakiwaambia: "Nyinyi si chochote isipokuwa ni wanaadamu mfano wetu." Yaani, basi vipi mnakuwa bora zaidi yetu kwa unabii na utume? "Mnataka kutuzuia yale waliyokuwa wakiabudu baba zetu?" Basi vipi tuache rai na mwenendo wa baba zetu kwa rai yenu? Na vipi tuwatii nyinyi ilhali nyinyi ni binadamu mfano wetu? "Basi tuleteeni hoja iliyo wazi;" yaani, hoja na ushahidi ulio wazi. Na kwa hili walikuwa wanakusudia ushahidi ambao wanaupendekeza wao. Vinginevyo, hakika ilikwisha tangulia kwamba Mitume wao waliwajia na hoja zilizo wazi.