يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱذْهَبُوا۟ بِقَمِيصِى هَـٰذَا فَأَلْقُوهُ عَلَىٰ وَجْهِ أَبِى يَأْتِ بَصِيرًا وَأْتُونِى بِأَهْلِكُمْ أَجْمَعِينَ ٩٣
{93} Yaani, Yusuf, amani iwe juu yake, aliwaambia ndugu zake: “Nendeni na shati langu hili na mlitupe usoni mwa baba yangu, atakuwa mwenye kuona,” kwa sababu kila ugonjwa una unatibiwa na kinyume chake. Basi shati hili lilipokuwa na athari za harufu ya Yusuf, ambayo iliujaza moyo wa baba yake kwa huzuni na hamu kubwa ambayo Mwenyezi Mungu tu ndiye anaijua vyema, alitaka ainuse ili roho yake imrudie, kisha nafsi yake imrudie, nafsi kuona kwake pia kumrudie. Na Mwenyezi Mungu ana hekima yake na siri mbalimbali katika hilo ambazo hawazijui waja wake, na Yusuf aliweza kujua kitu kuhusiana na jambo hili. "Na mnijie na ahali zenu wote.” Yaani, watoto wenu, na ukoo wenu, na wote wanaowafuta ili kukutana kwote kufanyike, na muondokewe na shida za maisha na ufinyu wa riziki.