يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰبَنِىَّ ٱذْهَبُوا۟ فَتَحَسَّسُوا۟ مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَا۟يْـَٔسُوا۟ مِن رَّوْحِ ٱللَّهِ ۖ إِنَّهُۥ لَا يَا۟يْـَٔسُ مِن رَّوْحِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلْقَوْمُ ٱلْكَـٰفِرُونَ ٨٧
{87} Yaaqub, amani iwe juu yake, aliwaambia wanawe: “Enyi wanangu! Nendeni mumtafute Yusuf na nduguye.” Yaani, fanyeni hima na jitahidini kuwatafuta, "wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu” kwa maana matumaini yanamlazimu mja kuwania na kujitahidi katika yale anayoyatarajia, na kukata tamaa kunamsababishia kuzembea na kufanya polepole. Na kitu kilicho bora zaidi ambacho waja wa Mwenyezi Mungu wanafaa kukitumaini ni fadhila yake, na ihsan yake na rehema yake, na faraja yake. "Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu makafiri.” Kwa kuwa, kwa sababu ya ukafiri wao wanaona kuwa rehema yake iko mbali, na kweli rehema yake iko mbali nao. Kwa hivyo msijifananishe na makafiri. Na hili lilionyesha kwamba matumaini ya mja juu ya rehema na faraja ya mja huwa kulingana na imani yake.