يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَدَخَلَ مَعَهُ ٱلسِّجْنَ فَتَيَانِ ۖ قَالَ أَحَدُهُمَآ إِنِّىٓ أَرَىٰنِىٓ أَعْصِرُ خَمْرًا ۖ وَقَالَ ٱلْـَٔاخَرُ إِنِّىٓ أَرَىٰنِىٓ أَحْمِلُ فَوْقَ رَأْسِى خُبْزًا تَأْكُلُ ٱلطَّيْرُ مِنْهُ ۖ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِۦٓ ۖ إِنَّا نَرَىٰكَ مِنَ ٱلْمُحْسِنِينَ ٣٦
{36} Yaani, "na" Yusuf alipoingia gerezani, "wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili" miongoni mwa wale walioingia humo. Kisha kila mmoja wao akaona ndoto, kwa hivyo wakamsimulia ndoto hizo Yusuf ili azifasiri. "Mmoja wao akasema: Hakika mimi nimeota kuwa ninakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Hakika mimi nimeota kuwa nimebeba mikate juu ya kichwa changu" na mkate huo "ndege wanakula kwayo. Hebu tuambie tafsiri yake." Yaani, tafsiri yake na namna mambo yao yatakavyoisha. Na kauli yao, "kwani sisi tunakuona wewe ni katika watu wazuri." Yaani, wewe ni katika watu wafanyao mazuri kwa waja. Basi tufanyie mazuri katika kututafsiria ndoto zetu kama ulivyowafayia mazuri wasiokuwa sisi. Kwa hivyo, wakamuomba Yusuf kupitia uzuri wake.