انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣٢

قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ ٱلَّذِى لُمْتُنَّنِى فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفْسِهِۦ فَٱسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَآ ءَامُرُهُۥ لَيُسْجَنَنَّ وَلَيَكُونًا مِّنَ ٱلصَّـٰغِرِينَ ٣٢

{32} Na ulipowadhihirikia uzuri dhahiri wa Yusuf, na wakapendezwa sana, na zikaonekana kwao udhuru nyingi zinazomuunga mkono mke wa mheshimiwa huyo, akataka kuwaonyesha uzuri wake wa ndani kwa kujisafisha kwake kukamilifu. Kwa hivyo akasema, akitangaza hilo na akieleza mapenzi yake makubwa, bila ya kujali, na tena kwa sababu lawama ile ya wanawake hao ilikuwa sasa imeondoka "Na kweli mimi nilimtaka naye akakataa." Yaani, alikataa lakini yeye ataendelea kumtaka kimapenzi, na kupita kwa wakati hakukumzidishia isipokuwa mapenzi, na hamu, na wasiwasi, na shauku kubwa ya mapenzi. Na ndiyo maana akamwambia Yusuf mbele yao: "Na asipofanya ninayomwamrisha, basi hapana shaka atafungwa gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio duni kabisa. ;" ili amlazimishe kwa kumtishia huku kumfanya ayafikie alichokusudia kutoka kwake.