يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
رَبِّ قَدْ ءَاتَيْتَنِى مِنَ ٱلْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِى مِن تَأْوِيلِ ٱلْأَحَادِيثِ ۚ فَاطِرَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ أَنتَ وَلِىِّۦ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ تَوَفَّنِى مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّـٰلِحِينَ ١٠١
{101} Mwenyezi Mungu alipomtimizia Yusuf yale aliyomtimizia kama vile kumuimarisha katika ardhi na utawala, na akayafurahisha macho yake kwa wazazi wake na ndugu zake, na baada ya elimu nyingi aliyopewa na Mwenyezi Mungu, akasema akiikiri neema ya Mwenyezi Mungu, akimshukuru kwa hilo, na akiomba uthabiti juu ya Uislamu, “Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa katika ufalme” na hayo ni kwa sababu alikuwa ni msimamizi wa hazina za ardhi na uendeshaji wake, na alikuwa waziri mkuu wa mfalme, “na umenifunza katika tafsiri ya mambo.” Yaani, ulinifundisha katika tafsiri ya mambo ya vitabu vilivyoteremshwa, na tafsiri ya ndoto na elimu nyinginezo. “Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! ... Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu.” Yaani, nidumishie Uislamu na uniimarishe juu yake mpaka unifishe ndani yake. Na hii haikuwa dua ya kujiharakishia kifo. “Na niunganishe na walio wema” miongoni mwa Manabii na walio wema na walio safi na walio bora.