انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · هود
السورة ١١

هود

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٣

قَالَ يَـٰقَوْمِ أَرَءَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّى وَءَاتَىٰنِى مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِى مِنَ ٱللَّهِ إِنْ عَصَيْتُهُۥ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِى غَيْرَ تَخْسِيرٍ ٦٣

{63} Na kwa madai yao kwamba lau wangelijua usahihi wa yale aliyowalingania, basi wangemfuata, na ilhali wao ni waongo katika hilo. Na ndiyo maana akaeleza uongo wao katika kauli yake. "Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi" yaani niko na hoja na yakini {naye akawa amenipa rehema kutoka kwake" Yaani, amenineemesha kwa ujumbe wake na wahyi wake. Yaani, Je, niwafuate katika hayo mliyo juu yake na yale mnayoniitia? "Je, ni nani atakayeninusuru kutokana na Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamnizidishii isipokuwa kuhasirika tu." Yaani, isipokuwa hasara tu, na maangamio, na madhara.