هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَآ إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا۟ مِنْهُ ۚ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ٥
{5} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ujinga wa washirikina na ukubwa wa upotovu wao kwamba "wanafunika vilivyomo vifuani mwao." Yaani, wanavigeuza ili wamfiche Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, vifua vyao vinakuwa vimezuiliwa mbali namna ya kwamba Mwenyezi Mungu hajui hali zao wala hawezi kuona sura zao. Yeye Mtukufu Akasema akibainisha kosa lao katika dhana hii: "Jueni kuwa wanapojigubika nguo zao" anawajua katika hali hiyo ambayo ni miongoni mwa vitu vilivyofichikana zaidi. Bali "Anajua yale wanayoyaficha" miongoni mwa maneno na vitendo "na yale wanayoyaweka hadharani" miongoni mwa hayo. Bali hata yale yaliyo zaidi ya hayo, ambayo ni kwamba "Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi yaliyomo vifuani." Yaani, yale yaliyo ndani yake miongoni mwa nia mbalimbali, na wasiwasi, na fikiria ambazo hawakuzitamka kwa siri au kwa sauti kubwa. Basi vipi hali yenu itafichikana kwake mnapovifunika vifua vyenu ili mjifiche kutoka kwake? Na inawezekana kwamba maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu anataja kupeana mgongo kwa wanaomkadhibisha Mtume, ambao wameghafilika na wito wake, kwamba kwa sababu ya ukubwa wa kupeana kwao mgongo wanavifunika vifua vyao. Yaani, wanajikunja wanapomuona Mtume, ili asiwaone na kuwaskizisha wito wake na kuwaaidhi kwa yenye kuwanufaisha. Basi Je, kuna kitu chochote juu ya kupeana mgongo huku? Kisha akawaonya kwamba Yeye Mtukufu anazijua hali zao zote na kwamba hawafichikani kwake, na atawalipa kwa matendo yao.