هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالَ رَبِّ إِنِّىٓ أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْـَٔلَكَ مَا لَيْسَ لِى بِهِۦ عِلْمٌ ۖ وَإِلَّا تَغْفِرْ لِى وَتَرْحَمْنِىٓ أَكُن مِّنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٤٧
{47} Basi hapo Nuhu - amani iwe juu yake - akajuta kujuta kukubwa kwa yale aliyoyafanya, na "akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nikuombe nisilo na elimu nalo. Na kama hunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika waliohasiri." Kwa hivyo, kwa njia ya msamaha na rehema, mja huokoka kutokana na kuwa miongoni mwa waliohasirika. Na hili liliashiria kuwa Nuhu - amani iwe juu yake - alikuwa hajui kuwa kumwomba Mola wake Mlezi kuhusu kumuokoa mwanawe kuliharamishwa na kunaingia katika kauli yake: "Wala usiniongeleshe kuwatetea wale waliodhulumu. Kwani, hao bila ya shaka watazamishwa." Bali mambo hayo mawili yalihitilafiana kwake, na akadhania kuwa alijumuishwa katika kauli yake: "Na ahali zako," lakini baada ya haya ikambainikia kuwa aliingia katika wale ambao ilikakatazwa kuwaombea dua, na kurejea kwa Mwenyezi Mungu kuhusiana nao.