هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُۥ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ٱبْنِى مِنْ أَهْلِى وَإِنَّ وَعْدَكَ ٱلْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ ٱلْحَـٰكِمِينَ ٤٥
{45} "Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi akasena: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ndiyo ya haki." [Yaani], Na ulikuwa umeniambia: basi beba humo katika kila jozi mbili dume na jike na ahali zako, wala hutayavunja yale uliyoniahidi. Labda yeye - rehema na amani ziwe juu yake - alisukumwa na huruma kubwa, na kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amemuahidi kuwaokoa ahali zake - na akadhani kwamba ahadi hiyo ilikuwa kwa ujumla wao; wale waliamini na wale ambao hawakuamini. Basi kwa sababu ya hilo, ndiyo akamwomba Mola wake Mlezi kwa dua hiyo, lakini pamoja na hayo, aliliachia jambo hilo hekima kuu ya Mwenyezi Mungu.