هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ ٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّجْمُوعٌ لَّهُ ٱلنَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ ١٠٣
{103} "Hakika katika hayo" yaliyotajwa miongoni mwa kuwaadhibu kwake madhalimu kwa aina mbali mbali za adhabu, "ipo ishara kwa yule anayehofu adhabu ya Akhera." Yaani, kuna mazingatio na ushahidi kwamba madhalimu na wahalifu wana adhabu ya kidunia na adhabu ya kiakhera. Kisha akatoka katika haya hadi katika kuielekeza Akhera, akasema: "Hiyo ndiyo Siku itakayokusanyiwa watu;" yaani, watakusanywa kwa ajili ya siku hiyo kwa ajili ya malipo na ili uwadhihirikie ukuu wa Mwenyezi Mungu, na mamlaka yake, na uadilifu wake mkuu jambo ambalo kwalo watajua kujua kwa haki "na hiyo ndiyo Siku itakayoshuhudiwa." Yaani, ataishuhudia Mwenyezi Mungu na Malaika wake na viumbe vyote.