الفيل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصْحَـٰبِ ٱلْفِيلِ ١ أَلَمْ يَجْعَلْ كَيْدَهُمْ فِى تَضْلِيلٍ ٢ وَأَرْسَلَ عَلَيْهِمْ طَيْرًا أَبَابِيلَ ٣ تَرْمِيهِم بِحِجَارَةٍ مِّن سِجِّيلٍ ٤ فَجَعَلَهُمْ كَعَصْفٍ مَّأْكُولٍۭ ٥
{1 - 5} Yaani: Je, hukuona katika uweza wa Mwenyezi Mungu, na ukuu wa jambo lake, na rehema zake kwa waja wake, na ushahidi wa upweke wake, na ukweli wa Mtume wake [Muhammad] - rehema na amani zimfikie - kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwafanyia watu wa tembo, ambao waliifanyia njama Nyumba yake Takatifu, na wakataka kuiharibu. Kwa hivyo wakajitayarisha kwa ajili ya hayo, na wakachukua pamoja nao tembo kwenda kuibomoa, wakaja na kundi ambalo Waarabu hawakuwa na uwezo wa kukabiliana nalo kutoka Uhabeshi na Yemeni. Walipofika karibu na Makka - na Waarabu hawakuwa na ulinzi, na watu wa Makka wakaondoka Makka kwa kujihofia nafsi zao kwa sababu yao, basi Mwenyezi Mungu akawatumia ndege makundi kwa makundi, huku wakibeba mawe ya udongo yaliyotiwa moto kutoka Motoni, wakawatupia hayo, na yakawafuatilia wa mbali wao na wa karibu wao, kwa hivyo wakafa na kuzimia, na wakawa kama majani yaliyoliwa, na Mwenyezi Mungu akawatosheleza watu wa Makka kutokana na maovu yao, na akazirudisha njama zao kooni mwao, na kisa chao hiki kinajulikana sana, na huo ndio mwaka aliozaliwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – na hilo likawa miongoni mwa dalili za wito wake na ushahidi wa ujumbe wake. Basi sifa njema na shukrani ni za Mwenyezi Mungu.