انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٥

وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ فَتَكُونَ مِنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٩٥

{95} "Na kabisa usiwe miongoni mwa wale waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, ukawa katika waliohasiri." Na muhtasari wa haya ni kwamba Mwenyezi Mungu alikataza mambo mawili: kuitilia shaka Qur-ani hii, na kusitasita juu yake. Na baya zaidi kuliko hayo ni kuikadhibisha. Nayo ndiyo ishara za wazi wazi za Mwenyezi Mungu, ambazo hazikubali kukadhibishwa kwa namna yoyote ile. Na alifungamanisha na hilo kupata hasara. Nayo ni kutokapa faida yoyote. Na hilo linakuwa kwa kukosa malipo katika dunia hii na Akhera, na kufikiwa na adhabu katika dunia hii na Akhera. Na kukataza kitu ni kuamrisha kinyume chake. Kwa hivyo inakuwa hii ni kuamrisha kuisadiki Qurani kikamilifu, na kuutuliza moyo juu yake, na kuielekea kwa kujifunza na kuitendea kazi. Na kwa hayo mja anakuwa miongoni mwa waliofaidika, ambao walipata mambo matukufu zaidi yatafutwayo, na matashi bora zaidi, na sifa (fadhila) kamili zaidi, na kuepushwa na hasara.