يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ثُمَّ بَعَثْنَا مِنۢ بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَـٰرُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ بِـَٔايَـٰتِنَا فَٱسْتَكْبَرُوا۟ وَكَانُوا۟ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ ٧٥
{75} Yaani: Kisha tukatuma baada ya Mitume hao ambao Mwenyezi Mungu aliwatuma kwa kaumu waliokadhibisha, walioangamizwa "Musa" Ibn Imran, aliyezungumza moja kwa moja na Mwingi wa rehema, mmoja wa Mitume wenye azimio kubwa miongoni mwa Mitume, na mmoja wa wakubwa wanaoigwa, walioteremshiwa sheria zilizo kuu na pana. "Na" tukamfanya pamoja naye nduguye "Harun" kuwa msaidizi. Na tukawatuma "kwa Firauni na waheshimiwa wake;" yaani, wakuu wa nchi yake na viongozi wao. Kwa sababu wengineo wote wanawafuata viongozi, "kwa Ishara zetu," zinazoonyesha ukweli wa yale aliyokuja nayo ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na kukataza kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Wakatakabari" juu yake kwa dhulumu tu na jeuri baada ya kuwa na yakini nayo. "Na wakawa kaumu wahalifu;" yaani, sifa yao ni kufanya uhalifu na kukadhibisha.