يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ ٱلْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ ٦٥
{65} Yaani, usihuzunishwe na maneno ya wale wanaokukadhibisha, ambayo kwayo wanafikia kukutia doa, na pia Dini yako. Kwa maana, maneno yao hayo hayawapi utukufu wala hayakudhuru hata kidogo. "Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu." Humpa huo amtakaye na humnyima amtakaye. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, "Mwenye kutaka utukufu, basi utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu." Yaani na autafute katika kumtii, kwa ushahidi wa kauli yake baada yake: "Kwake Yeye hupanda neno zuri, na tendo jema Yeye hulitukuza." Na inavyojulikana ni kwamba wewe unamtii Mwenyezi Mungu, na kwamba utukufu ni wako na wa wafuasi wako kutoka kwa Mwenyezi Mungu. "Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu, na Mtume wake, na Waumini." Na kauli yake, "Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema Mwenye kujua yote." Yaani, kusikia kwake kulizunguka sauti zote, kwa hivyo hakifichiki kitu kwake. Na elimu yake imezunguka kila ya dhahiri na ya ndani. Basi hakifichikani kwake chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na mbingu, wala kidogo zaidi kuliko hicho wala kikubwa zaidi. Na Yeye Mtukufu anayasikia maneno yako na maneno ya maadui zako kukuhusu wewe. Na anayajua hayo kwa kina. Kwa hivyo tosheka na elimu ya Mwenyezi Mungu na kutosheleza kwake. Kwa hivyo, mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, basi Yeye anamtosha.