انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٣

وَيَسْتَنۢبِـُٔونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِى وَرَبِّىٓ إِنَّهُۥ لَحَقٌّ ۖ وَمَآ أَنتُم بِمُعْجِزِينَ ٥٣

{53} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake -rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - "Na wanakuuliza, "Je, ni kweli hayo?" Yaani, hao wakadhibishaji wanataka kujua kutoka kwako kwa njia ya inda na ukaidi, si kwa njia kutaka kubainshiwa na kutafuta mwelekeo, "Je, ni kweli hayo?" Yaani, je ni sahihi kwamba waja watakusanywa pamoja na kufufuliwa baada ya kufa kwao kwa ajili ya Siku ya Kiyama, na kwamba waja watalipwa kwa matendo yao, ikiwa ni heri, basi kwa heri, na ikiwa maovu, basi kwa maovu? "Sema," uwaambie ukiapa juu ya usahihi wake, na kwa kuweka ushahidi wazi na hoja juu ya hilo: "Ehe! Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika hayo ni kweli" Hakuna shaka yoyote ndani yake wala mchanganyiko wowote ndani yake, "na wala nyinyi hamtamshinda" Mwenyezi Mungu kuwafufua. Kwani, kama alivyoanzisha kuwaumba nyinyi, nanyi hamkuwa kitu, basi vivyo hivyo atawarejesha mara nyingine ili awalipe kwa matendo yenu.