يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَهْدِىٓ إِلَى ٱلْحَقِّ ۚ قُلِ ٱللَّهُ يَهْدِى لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَن يَهْدِىٓ إِلَى ٱلْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا يَهِدِّىٓ إِلَّآ أَن يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ ٣٥
{35} "Sema, "Je, yupo yeyote katika washirika wenu mwenye kuongoa kwenye haki?" Kwa kubainisha kwake na kuelekeza kwake au kwa ufunuo (wahyi) wake na kuwezesha kwake? “Sema, "Mwenyezi Mungu" peke yake "anaongoa" kwenye haki kwa ushahidi na hoja na ufunuo na kuwezesha, na usaidizi wa kushika njia iliyonyooka zaidi. "Au yule asiyeongoka;” yaani, haongoki "isipokuwa akiongozwa," kwa sababu ya kutojua kwake na kwa sababu ya upotofu wake. Nao ni hao washirika wao ambao hawaongoi wala hawaongoki isipokuwa wakiongozwa. "Basi nyinyi mna nini, mnahukumu namna gani?” Yaani, ni kitu gani kiliwafanya mnahukumu hukumu hii batili ya kwamba ni sahihi kumuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu baada ya kudhihirika kwa hoja na ushahidi kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake? Na inapobainika kwamba hakuna katika miungu yao wanayoiabudu pamoja na Mwenyezi Mungu sifa za kimaana wala sifa za kimatendo zinazolazimu waabudiwe pamoja na Mwenyezi Mungu, bali hao wanasifika kwa upungufu wenye kulazimu ubatili wa uungu wao; basi ni kwa kitu gani walifanywa kuwa waungu pamoja na Mwenyezi Mungu?