انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٤

إِنَّمَا مَثَلُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا كَمَآءٍ أَنزَلْنَـٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخْتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ ٱلنَّاسُ وَٱلْأَنْعَـٰمُ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَخَذَتِ ٱلْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَٱزَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَآ أَنَّهُمْ قَـٰدِرُونَ عَلَيْهَآ أَتَىٰهَآ أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا فَجَعَلْنَـٰهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِٱلْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ٢٤

{24} Na mfano huu ni katika mifano mizuri zaidi, ambao unaingiana sawa sawa na hali ya dunia hii; kwa maana, raha zake, na matamanio yake, na heshima yake, na mfano wa hayo yanampendeza mwenyewe yanapompendeza kwa muda mfupi, na yanapokamilika na yakatimia, yanafifia na kutoweka kwa mwenyewe au mwenyewe anayaacha. Kwa hivyo, akawa mikono mitupu bila ya hayo, huku amejaa moyo na wasiwasi mkubwa juu yake, na huzuni yake na majuto yake, basi hayo ni "kama maji tuliyoyateremsha kutoka mbinguni, kisha mimea ya ardhi.” Yaani, ikaota kutoka humo kila aina na jozi nzuri, "miongoni mwa vile wanayvovila watu” kama vile nafaka na matunda, "na" katika vile wanavyovila "wanyama" kama vile aina mbalimbali za nyasi na malisho ya sampuli tofauti tofauti. "Mpaka ardhi ilipokamilika uzuri wake, na ikapambika;” yaani, ikapambwa katika mwonekano wake na ikavalika kwa mapambo yake, kwa hivyo ikawa nzuri kwa watazamaji, na matembezi ya burudani kwa wafurahiao, na ishara kwa wenye kuona, kisha ukaanza kuiona katika mtazamo wa ajabu kama vile kijani, njano, nyeupe na mingineyo. “Na wenyewe wakadhani kwamba wameshaiweza;” yaani, wakawa na matumaini kwamba hayo yataendelea na kudumu, kwa sababu matashi yao yalisimamia hapo, na yale wanayoyatafuta yakaishia humo. Na walipokuwa katika hali hiyo, amri ya Mwenyezi Mungu ikaijia “usiku au mchana, kwa hivyo tukaifanya kama iliyofyekwa, kama kwamba haikuwapo jana;” basi hii ndiyo hali ya dunia hii mia kwa mia. "Hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara zetu;” yaani, tunazibainisha na kuziweka wazi kwa kuleta maana karibu na akili na kuzipigia mifano, "kwa kaumu wanaotafakari.” Yaani, wanatumia fikira zao katika yale yenye kuwanufaisha. Na ama aliyeghafilika, aliyepeana mgongo, basi huyu hazimnufaishi ishara, na kubainisha hakumuondolei shaka yake.