انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٨

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰٓؤُلَآءِ شُفَعَـٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ١٨

{18} Yeye Mtukufu anasema: "Na wanaabudu;" Yaani, washirikina wanaomkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie – "badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha.“ Yaani, hawawamilikii uzito wa chembe ya manufaa, wala hawawazuilii chochote. "Na wanasema” maneno yasiyo na ushahidi: "Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu” Yaani, wanawaabudu ili kuwakurubishe kwa Mwenyezi Mungu na wawafanyie uombezi kwake. Na hii ni kauli kutoka tu kwao wenyewe. Na ni kauli waliyoizua wao, na ndiyo maana Akasema, akibatilisha kauli yao hii: "Sema, “Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi?” Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mwenye kujua yote ambaye amekizunguka kwa elimu kila kitu kilicho katika mbingu na ardhi. na tayari alikwisha wajulisha kwamba hana mshirika yeyote wala hana mungu yeyote pamoja naye. Basi enyi kundi la washirikina mnadai kuwa anao washirika ndani yake. Kwani mnamwambia jambo ambalo limefichikana kwake lakini nyinyi mkalijua? Je, nyinyi ndio mnaojua au Mwenyezi Mungu? Basi Je, kuna kauli batili zaidi kuliko kauli hii inayojumuisha kwamba hawa wapotofu, wajinga, na wapumbavu ni wenye kujua zaidi kuliko Mola Mlezi wa walimwengu wote? Basi Mwenye akili na atosheke na kufikiria tu kauli hii; kwani atakuwa na uhakika juu ya ubovu wake na ubatili wake. "Ametakasika na ametukuka na hao wanaomshirikisha naye.” Yaani, ametakasika na ametukuka kuwa na mshirika au mwenza. Bali Yeye ni Mwenyezi Mungu, Mmoja, wa kipekee, Mkusudiwa ambaye hakuna Mungu katika mbingu na ardhi isipokuwa Yeye. Na kila muabudiwa katika ulimwengu wa juu na wa chini asiyekuwa Yeye ni batili, kiakili, na kisheria, na kimaumbile. "Hayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa haki, na kwamba wale wanaowaomba badala yake, ni baatili, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Aliye Juu na ndiye Mkubwa.“