U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Suuradda 9

At-Tawba

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 24

قُلْ إِن كَانَ ءَابَآؤُكُمْ وَأَبْنَآؤُكُمْ وَإِخْوَٰنُكُمْ وَأَزْوَٰجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَٰلٌ ٱقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَـٰرَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَـٰكِنُ تَرْضَوْنَهَآ أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَجِهَادٍ فِى سَبِيلِهِۦ فَتَرَبَّصُوا۟ حَتَّىٰ يَأْتِىَ ٱللَّهُ بِأَمْرِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ 24

{24} Na ndiyo maana akataja sababu inayoleta hilo. Nayo ni kwamba upendo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ni lazima kuutanguliza mbele ya upendo kwa vitu vyote, na kufanya vitu vyote viwe vyenye kufuata hayo. Kwa hivyo akasema, "Sema: Ikiwa baba zenu" na mfano wao ni kina mama, "na ndugu zenu;" katika nasaba na kwa sababu ya kuishi pamoja "na wake zenu, na jamaa zenu." Yaani, jamaa zenu kwa ujumla, "na mali mlizozichuma," yaani, ulizozichuma na kutaabika katika kuzipata. Na alizitaja hasa kwa sababu ndizo zinazotakiwa zaidi kwa wenyewe, na mwenyewe anaitunza kwa juhudi kubwa kuliko yule ambaye mali zinamjia bila taabu wala shida. Na hili linajumuisha biashara zote miongoni mwa vitu vya thamani, na vyombo, na silaha, na bidhaa, na nafaka, na mashamba, na mifugo na kadhalika. "Na makazi mnayoyaridhia" kwa sababu ya uzuri wake na mapambo yake na kuafikiana kwake na matamanio yenu. Basi ikiwa vitu hivi "ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya Jihadi katika Njia yake," basi nyinyi mmevuka mipaka, ni madhalimu. "Basi ngojeni;" yaani, yangojeni yale yatakayowafika ya adhabu "mpaka Mwenyezi Mungu aje na amri yake" ambayo haiwezi kurudishwa. "Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka." Yaani, wale wanaotoka katika utiifu wake, wanaotanguliza mbele ya kumpenda Mwenyezi Mungu kitu katika yale yaliyotajwa. Na Aya hii tukufu ni ushahidi mkubwa zaidi juu ya ulazima wa kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na juu ya kuwatanguliza mbele ya kupenda kila kitu katika vitu, na juu ya ahadi ya adhabu kali, na chukizo la kweli kwa yule mabye kitakuwa kitu chochote katika [hivi] vilivyotajwa ni pendwa zaidi kwake kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Jihadi katika njia yake. Na alama ya hilo ni kwamba ikiwa atawekewa mambo mawili: moja yake analipenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na nafsi yake haina matamanio nalo, na lingine nafsi yake inalipenda, na inalitaka, lakini linampotezea kile anachokipenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake au linakipunguza. Basi ikiwa atatanguliza kile inachopenda nafsi yake mbele ya kile anachokipenda Mwenyezi Mungu, basi hilo litaashiria kuwa yeye ni dhalimu, mwenye kuacha kile cha wajibu juu yake.