U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Suuradda 9

At-Tawba

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 111

إِنَّ ٱللَّهَ ٱشْتَرَىٰ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَٰلَهُم بِأَنَّ لَهُمُ ٱلْجَنَّةَ ۚ يُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِى ٱلتَّوْرَىٰةِ وَٱلْإِنجِيلِ وَٱلْقُرْءَانِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِۦ مِنَ ٱللَّهِ ۚ فَٱسْتَبْشِرُوا۟ بِبَيْعِكُمُ ٱلَّذِى بَايَعْتُم بِهِۦ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ 111

{111} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu habari ya ukweli na anaahidi ahadi ya kweli ya biashara kubwa na ubadilishanaji mkubwa. Nayo ni kwamba, Yeye kwa nafsi yake tukufu "alinunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao," ambazo ndizo thamani na bidhaa zinazouzwa "kwa kuwa wao wana Pepo" ambayo ndani yake kuna kila aina ya vitu vinavyotamaniwa na nafsi na kupendeza macho miongoni mwa aina mbalimbali za raha, na furaha, na yafurahishayo, na hurulaini wazuri, na nyumba nzuri nzuri. Na namna ya mkataba huo na biashara hiyo ni kwamba wampe Mwenyezi Mungu roho zao na mali zao katika kufanya jihadi dhidi ya maadui zake, kwa ajili ya kuinua neno lake na kudhihirisha dini yake. Basi wanapigana vita "katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanaua na wanauawa.” Basi mkataba huu na biashara hii vilitoka kwa Mwenyezi Mungu vikiwa vimesisitizwa kwa aina mbalimbali za kusisitiza. "Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa haki katika Taurati, na Injili, na Qur-ani” ambayo ndicho kitukufu zaidi ya vitabu vyote, ambacho kilikuja katika ulimwengu, na cha juu chake zaidi, na kikamilifu chake zaidi. Na alikuja nacho aliye mkamilifu zaidi wa Mitume wote, wenye azimio kubwa. Navyo vyote vilikubaliana juu ya ahadi hii ya ukweli. "Na nani atimizaye zaidi ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini” enyi Waumini, mnaotekeleza yale aliyowaahidi Mwenyezi Mungu “kwa biashara yenu mliyofanya naye.” Yaani, furahieni hilo, na peaneni bishara njema nyinyi kwa nyinyi. "Na huko ndiko kufuzu kukubwa” ambako hakuna kufuzu kukubwa kuliko huko, wala kutukufu zaidi yake. Kwa sababu kunajumuisha furaha ya milele, na neema ya kudumu, na ridha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ambayo ndiyo kubwa zaidi kuliko neema ya mabustani ya mbinguni. Na ukitaka kujua kiasi cha mapatano haya, basi mwangalie yule anayenunua. Yeye ni nani? Yeye ni Mwenyezi Mungu, mwenye utukufu mkubwa. Na tazama malipo yake. Hayo ndiyo makubwa zaidi ya malipo yote na tukufu yake zaidi, ambayo ni mabustani ya neema. Na tazama thamani iliyotolewa katika hilo, ambayo ni nafsi na mali, ambavyo ndivyo vitu vinavyopendwa zaidi na mwanadamu. Na tazama yule ambaye mkataba huu ulikamilishwa katika mikono yake. Yeye ndiye mtukufu zaidi miongoni mwa Mitume. Na hilo liliandikwa katika kitabu gani? Ni katika vitabu vikubwa vya Mwenyezi Mungu vilivyoteremshwa juu ya wabora zaidi wa viumbe wote.