Al-Ghaashiya
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَـٰشِعَةٌ 2 عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ 3 تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً 4 تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ ءَانِيَةٍ 5 لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ 6 لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِى مِن جُوعٍ 7
{2 - 7} Basi akasema katika kuwaelezea watu wa Motoni: "Siku hiyo" ya Kiyama "nyuso zitainama" kutokana na fedheha na hizaya "Zikifanya kazi, nazo taabani" na zitahangaika katika adhabu, huku wakiburutwa "na Moto utazigubika nyuso zao." Na inawezekana kwamba kile kinachomaanishwa na kauli yake: “Siku hiyo nyuso zitainama. Zikifanya kazi, nazo taabani" kwa sababu walifanya ibada na matendo katika dunia hii, lakini hayakuwa yameambatana na masharti yake, ambayo ni imani; basi Siku ya Kiyama yakawa mavumbi yaliyotawanywa. Ingawa uwezekano huu ni sahihi katika maana yake, lakini muktadha wa mazungumzo hayaionyeshi. Bali maana sahihi ya uhakika ni ile maana ya kwanza. Kwa sababu aliiwekea mipaka ya wakati, yaani Siku ya Kiyama, na kwa sababu kinachokusudiwa hapa ni kueleza watu wa Motoni kwa ujumla, na uwezekano huo ni sehemu ndogo tu kuhusiana na watu wa Motoni, na kwa sababu mazungumzo haya yanaelezea hali ya watu watakapojiwa na msiba mkubwa, na hayaashirii hali zao katika dunia hii. Na kauli yake: "Ziingie katika Moto unaowaka" utakaowazunguka kutokea kila mahali, "Zikinyweshwa kutoka chemchemi inayochemka" sana "Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyotibuka. Yatayo wababua nyuso zao." Hiki ndicho kinywaji chao, na ama chakula chao; “Hawatakuwa na chakula isipokuwa kichungu chenye miba. Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa" Haya ni kwa sababu makusudio ya chakula ni moja ya mambo mawili: ima kukidhi njaa ya mtu na kumpunguzia maumivu yake, au kuufanya mwili wake unenepe na kutodhoofika. Na chakula hiki hakina chochote katika vitu hivi viwili. Badala yake, ni chakula kichungu mno, kinachonuka na kibaya sana. Tunamuomba Mwenyezi Mungu salama.