U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Suuradda 6

Al-An'aam

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 93

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِىَ إِلَىَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَىْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّـٰلِمُونَ فِى غَمَرَٰتِ ٱلْمَوْتِ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ بَاسِطُوٓا۟ أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوٓا۟ أَنفُسَكُمُ ۖ ٱلْيَوْمَ تُجْزَوْنَ عَذَابَ ٱلْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ غَيْرَ ٱلْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ ءَايَـٰتِهِۦ تَسْتَكْبِرُونَ 93

{93} Yeye Mtukufu Anasema, hakuna aliye dhalimu mkubwa zaidi wala mhalifu mkubwa zaidi kuliko yule anayemsingizia uongo Mwenyezi Mungu, kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu neno au hukumu ilhali Yeye mtukufu yuko mbali nayo. Na huyu ndiye dhalimu zaidi katika viumbe kwa sababu, ndani ya hilo kuna uongo na kubadili dini mbalimbali, na misingi yake, na matawi yake; na kunasibisha hayo na Mwenyezi Mungu, ambayo ni miongoni mwa maharibifu makubwa zaidi. Na inaingia katika hili kudai unabii, na kwamba Mwenyezi Mungu humteremshia wahyi, ilhali yeye ni mwongo katika hilo. Kwani, pamoja na uongo wake juu ya Mwenyezi Mungu na ujasiri wake juu ya ukuu wake na mamlaka yake, yeye anawawajibishia watu kumfuata, na anapigane nao vita juu ya hilo, na anahalalisha damu ya mwenye kumhalifu, na mali zao. Na anaingia katika Aya hii kila aliyedai unabii, kama vile Musaylimah Mwongo mkubwa, na Al-Aswad Al-‘Ansi, na Al-Mukhtar, na wengineo ambao miongoni mwa wale walioelezewa kwa maelezo haya. "Na yule anayesema: Nitateremsha mfano wa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu." Yaani, ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayedai kuwa yeye ni muweza wa kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu anayaweza, na anafanya pamoja na Mwenyezi Mungu katika hukumu zake, na anaweka sheria miongoni mwa sheria mbalimbali kama vile Mwenyezi Mungu anavyoweka sheria? Na anaingia katika hili kila anayedai kwamba ana uwezo wa kuipinga Qur-aani, na kwamba anaweza kuleta mfano wake! Na je, ni dhuluma gani kubwa zaidi kuliko kudai kwamba fakiri, asiyejiweza yeye mwenyewe, mpungufu katika kila njia, kushirikiana Mwenye nguvu, anayejitosheleza ambaye ana ukamilifu wote katika kila njia, katika dhati yake, na majina yake, na sifa zake? Na alipotaja shutuma juu ya madhalimu, Akataja adhabu aliyowaandalia katika hali ya kufa na Siku ya Qiyama. Kwa hivyo akasema, "Na lau ungeliwaona madhalimu wanapokuwa katika mahangaiko ya mauti; yaani, taabu zake, na ugumu wake wa kutisha, na dhiki yake mbaya, basi ungeliona jambo kubwa na hali ambayo hawezi mwenye kueleza kuieleza. "Malaika wamewanyooshea mikono yao" madhalimu hao wanaokufa kwa kupiga na kuadhibu, na wanawaambia wakati wa kutoa roho zao, na wasiwasi wake, na kukataa kwake kutoka katika miili yao: "Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya kudunisha." Yaani, adhabu kali ambayo itawadunisha na kuwadhalilisha. Na malipo ni ya aina sawa na matendo. Kwani adhabu hii ni "kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki;" miongoni mwa kumsingizia kwenu uwongo na kuikataa kwenu haki ambayo walikuja nayo Mitume. "Na mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake," yaani mnajiinua juu kwa kukataa kuzifuata na kujisalimisha kwa hukumu zake. Na katika hili kuna ushahidi juu ya adhabu ya Barzakh (kaburini). Kwa maana, maneno haya na adhabu yanayoelekezwa kwao ni wakati wa kufa tu, kabla ya kufa na baada yake. Na ndani yake kuna ushahidi kwamba roho ni mwili unaoingia, na unatoka, na unaongeleshwa, na unakaa ndani ya mwili, na kuuacha.