Al-An'aam
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَعِندَهُۥ مَفَاتِحُ ٱلْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَآ إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ مُّبِينٍ 59
{59} Aya hii kubwa ni miongoni mwa Aya kubwa kabisa katika kubainisha elimu Yake iliyoenea kila kitu. Na kwamba Yeye imeizunguka ghaibu yote, ambayo Anaonyesha kwayo atakavyo kwa viumbe Vyake, na nyingi katika hiyo Ameificha elimu yake kutoka kwa Malaika wa karibu zaidi na Manabii waliotumwa; achilia mbali wasiokuwa wao miongoni mwa walimwengu wengine. Na kwamba, Yeye anayajua yaliyomo katika majangwa, na nyika miongoni mwa wanyama, na miti, na mchanga, na changarawe, na udongo, na vilivyomo ndani ya bahari miongoni mwa wanyama wake, madini yake, na mawindo yake, na vitu vinginevyo vilivyomo katika sehemu pande zake, na vinajumuishwa na maji yake. "Na halidondoki jani lolote," kutoka katika miti ya nchi kavu, na bahari, na miji mbalimbali, na nyika, na dunia, na Akhera, isipokuwa Analijua."Wala punje katika giza mbalimbali ya ardhi" miongoni mwa punje za matunda na mimea, na punje za mbegu ambazo viumbe wanazipanda, na mbegu za mimea ya porini ambazo kwazo zinatoka aina mbalimbali za mimea. "Wala kinyevu, wala kikavu. Huu ni jumla baada ya umaalumu "isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha;" ambacho ni Ubao uliohifadhiwa. Ambao Alivibeba na kuvijumuisha; na baadhi ya haya yaliyotajwa yanashangaza akili za watu wenye akili timamu, na yanashangaza nyoyo za watu watukufu. Kwa hivyo hili likaashiria ukubwa wa Mola Mlezi Mkuu na ukunjufu wake katika sifa zake zote, na kwamba viumbe tokea wa mwanzo wake hadi wa mwisho wake, lau watakusanyika ili wazunguke vyema baadhi ya sifa zake; hawangekuwa na nguvu zozote wala uwezo wa kufanya hivyo. Basi ni mwingi wa baraka Mola Mlezi Mkuu, Mwenye wasaa, Mwenye kujua yote, Msifiwa, Mheshimiwa, Mwenye kushuhudia yote, Mwenye kuzunguka vyote, na ametukuka Mungu hakuna anayeweza vyema kumsifu. Bali Yeye yuko vile alivyojisifu Mwenyewe, na juu ya vile waja Wake wanavyomsifu. Basi Aya hii iliashiria elimu Yake iliyokizunguka kila kitu na andiko lake lililoyazunguka matukio yote.