Al-An'aam
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
قُلْ يَـٰقَوْمِ ٱعْمَلُوا۟ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّى عَامِلٌ ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُۥ عَـٰقِبَةُ ٱلدَّارِ ۗ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ 135
{135} "Sema:" Ewe Mtume kwa kaumu yako, unapowalingania kwa Mwenyezi Mungu na ukawabainishia hatima yao na haki zake zilizo juu yao, lakini wakakataa kufuata amri yake, na wakafuata matamanio yao, na wakaendelea juu ya Ushirikina wao: "Enyi kaumu yangu! Fanyeni mahali penu mlipo." Yaani, katika hali yenu ambayo mmo, na mkairidhia nafsi zenu, "na hakika mimi ninafanya" kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na ninafuata anayoridhia Mwenyezi Mungu. "Mtakuja jua ni ya nani yatakuwa makaazi mema mwishoni;" mimi au nyinyi. Na huu ni miongoni mwa uadilifu katika mahali pakubwa. Ambapo alibainisha matendo na wanaoyafanya, na akafanya malipo kuwa yanafungamana na utambuzi wa Mwenye kuona, na akaacha kuisema kwa kauli ya waziwazi ambayo inatoshelezwa na kudokezwa tu. Na tayari ilikwisha julikana kwamba mwisho mzuri katika dunia na Akhera ni wa wachamungu, na kwamba Waumini ndio wenye nyumba ya mwisho iliyo bora, na kwamba kila mwenye kupeana mgongo kwa yale yaliyoletwa na Mitume mwisho wake ni mwisho mbaya na muovu. Na ndiyo maana akasema, "Hakika, madhalimu hawafaulu." Basi kila dhalimu, hata akistareheka katika dunia kwa yale anayostareheka kwayo, mwisho wake ni kupotea na kuharibika. Hakika Mwenyezi Mungu humpa muhula dhalimu, mpaka anapomkamata, hawezi kumkwepa.