At-Tur
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ ۖ وَزَوَّجْنَـٰهُم بِحُورٍ عِينٍ 20
{20} "Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyopangwa kwa safu." Na Mwenyezi Mungu amevielezea viti hivyo kwamba vilipangwa kwa safu ili hilo liashirie wingi wake, na uzuri wa mpangilio wake na mkusanyiko wa watu wake, na furaha yao kwa sababu ya kuishi kwao pamoja kwa uzuri, na kufanyiana kwao upole. Wakati furaha ya moyo, nafsi, na mwili ilipokusanyika kwa ajili yao, kutokana na yale yasiyofikirika akilini wala hata kuzunguka mawazani kama vile chakula kitamu na vinywaji, na mahali pa kukaa pazuri na ya kifahari, halikubakia lolote ila kustareheshwa kwa wanawake ambao kwamba haitimii furaha isipokuwa kwa hao. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja kwamba wana wake wakamilifu katika sifa zao, maumbile yao na maadili yao, na ndiyo maana akasema: "Na tutawaoza mahurulaini." Nao ni wanawake ambao wamekusanya uzuri wa sura ya nje na pamoja uzuri wake mkubwa, na ni wenye tabia njema ambayo kwayo inasababisha kuwachanganya wenye kutazama kwa sababu ya uzuri wake, na kukanganya akili za walimwengu, na mioyo inakaribia kuruka kwa hamu kubwa ya kuwataka na kuwafikia. Nao ni wenye macho mazuri yenye weupe na weusi uliobanika wazi.