Al-Maaida
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
مَّا ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ ٱلرُّسُلُ وَأُمُّهُۥ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ ٱلطَّعَامَ ۗ ٱنظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ ثُمَّ ٱنظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ 75
{75} Kisha akataja uhakika wa Masihi na mama yake, ambako ni kutaja kwa haki, kwa hivyo akasema; "Masihi mwana wa Maryam si chochote isipokuwa ni Mtume;" yaani, hiki ndicho kikomo chake na mwisho wa jambo lake. Kwamba yeye ni miongoni mwa waja waliotumwa na Mwenyezi Mungu, ambao hawana chochote katika jambo hilo wala katika sheria isipokuwa yale aliyowatuma nayo Mwenyezi Mungu. Naye ni wa aina moja na Mitume waliomtangulia, wala hana sifa maalum kuwashinda yenye kumtoa nje ya ubinadamu hadi daraja ya umola. "Na mama yake" Maryamu ni "mkweli;" yaani, hiki pia ndicho kikomo chake, kwamba alikuwa miongoni mwa wakweli, ambao ndio wa daraja la juu kabisa katika viumbe baada ya Mitume. Na ukweli ni elimu yenye manufaa yenye kuleta yakini na matendo mema .Na huu ni ushahidi kuwa Maryamu hakuwa Nabii, lakini hali yake ya juu zaidi ilikuwa ya ukweli, na hilo linatosha kuwa fadhila na heshima. Na kadhalika, wanawake wengineo wote, hakuna aliyekuwa Nabii miongoni mwao. Kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu aliufanya unabii kuwa katika lililo kamili zaidi kati ya aina hizo mbili; katika wanaume. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Na hatukuwatuma kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia." Kwa hivyo, ikiwa Isa , amani iwe juu yake, alikuwa wa aina sawa na Manabii na Mitume wa kabla yake, na mama yake alikuwa mkweli; basi ni wa kitu gani Wakristo waliwafanya wao wawili kuwa miungu wawili pamoja na Mwenyezi Mungu? Na kauli yake, “Wote wawili walikuwa wakila chakula” ni uthibitisho ulio dhahiri kuwa walikuwa waja maskini, wenye uhitaji, kama vile wanavyohitaji wanadamu wengineo chakula na vinywaji. Na lau kuwa wangekuwa ni miungu wawili, basi hawangehitaji chakula na vinywaji, na hawangehitaji chochote. Kwa maana Mungu ni yule ambaye hahitaji chochote, Msifiwa. Na Yeye Mtukufu alipobainisha ushahidi, Akasema, "Angalia jinsi tunavyowabainishia Aya" zinazobainisha haki na kuweza wazi yakini, lakini pamoja na hayo haziwanufaishi chochote, bali hawaachi kuwa katika uongo wao na uongo wao, na uzushi wao, na hilo ni dhuluma na ukaidi kutoka kwao.