U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zukhruf
Suuradda 43

Az-Zukhruf

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 81

قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلْعَـٰبِدِينَ 81

81 Yaani: Sema, ewe Mtume mtukufu ukiwaambia wale waliomfanyia Mwenyezi Mungu mwana, naye ndiye Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, ambaye hakujifanyia mke wala mwana, wala hana anayelingana naye hata mmoja. "Sema: 'Ingelikuwa Ar-Rahmani (Mwingi wa rehema) ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumuabudu.'" mwana huyo. Kwa sababu yeye ni sehemu ya baba yake, na mimi ndiye kiumbe anayestahiki zaidi kufuata maamrisho yanayopendwa na Mwenyezi Mungu. Lakini mimi ndiye wa kwanza kulikataa hilo, na mwenye kulikanusha zaidi yao wote, kwa hivyo ubatili wake ukajulikana kwa hilo. Hii ni hoja kubwa sana kwa wale wanaozijua hali za Mitume, na kwamba inapojulikana kuwa wao ndio viumbe kamili zaidi, na kwamba kila heri wao ndio wangekuwa watu wa kwanza kutangulia kuiendea na kuikamilisha, na kwamba kila uovu wao ndio wa kwanza kuuacha, kuukataa na kujiweka mbali nao. Kwa hivyo, kama Mwingi wa Rehema angekuwa na mwana, na hilo likawa ndiyo Haki, basi Muhammad bin Abdullah mbora wa Mitume wote angelikuwa ndiye wa kwanza kumuabudu, na wala washirikina wasingemtangulia katika hilo. Na inawezekana kwamba maana ya Aya ni kuwa: Lau Mwingi wa Rehema angekuwa na mwana, basi mimi ningekuwa ndiye wa kwanza kumwabudu Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwa kumwabudu kwangu Mwenyezi Mungu ni kuthibitisha yale aliyoyathibitisha na kukanusha yale aliyoyakanusha. Hii ni sehemu ya ibada ya kimaneno na kiitikadi, na inalazimu kutokana na haya kwamba ikiwa kweli ni haki, basi ningelikuwa wa kwanza kuyathibitisha. Basi ikajulikana kutokana na hilo ubatili wa madai ya washirikina ni ubovu wake kiakili na kimaandiko.