An-Nisaa
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَإِن مِّنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِۦ قَبْلَ مَوْتِهِۦ ۖ وَيَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا 159
{159} Na kauli yake, "Na hawi katika Watu wa Kitabu isipokuwa hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake." Inawezekana kwamba kiwakilishi ‘kwake’ hapa katika kauli yake ‘kabla ya kufa kwake inarejea kwa Watu wa Kitabu. Basi kama hivi inakuwa maana yake ni kwamba kila mtu wa Kitabu ambaye anahudhuriwa na mauti na akayaona mambo kwa uhakika, yeye hapo atamwamini Isa, amani iwe juu yake, lakini ni imani isiyofaa; ni Imani ya kulazimishwa. Kwa hivyo yanakuwa maudhui ya hili ni tishio na onyo la adhabu ili wasiendelee katika hali hii ambayo wataijutia kabla ya kufa kwao. Basi itakuwaje hali yao siku ya kukusanywa kwao na kufufuliwa kwao? Na Inawezekana kwamba kiwakilishi katika kauli yake “kabla ya kufa kwake” kinamrejelea Isa, amani iwe juu yake. Kwa hivyo maana yake inakuwa, hakuna hata mmoja katika Watu wa Kitabu isipokuwa atamwamini Masihi, amani iwe juu yake, kabla ya kifo cha Masihi. Na hilo litakuwa wakati Saa itakapokaribia na kuonekana kwa dalili zake kuu. Kwani kuna Hadithi nyingi Sahihi kuhusu kuteremka kwake, amani iwe juu yake, katika mwisho wa umma huu. Atamuua Dajjal na atasimamisha kutoa kwa Jizya (kodi anayoitoa asiyekuwa Muislamu katika nchi ya Waislamu kwa ajili ya kupewa ulinzi), na Watu wa Kitabu watamuamini pamoja na Waumini. "Naye Siku ya Qiyama," Isa atakuwa shahidi juu yao. Atashuhudia dhidi yao kwa vitendo vyao, na je vinaafikiana na sheria ya Mwenyezi Mungu au hapana? Na hapo, hatashuhudia isipokuwa ubatili wa kila kitu walicho juu yake ambacho ni kinyume na sheria ya Qur-ani, na kwa yale aliyowalingania Muhammad – swala na amani ziwe juu yake. Tulijua hilo kwa sababu ya elimu yetu juu ya uadilifu kamili wa Masihi amani ziwe juu yake na ukweli wake, na kwamba yeye hatashuhudia isipokuwa haki, isipokuwa kwamba yale aliyoyaleta Muhammad-rehema na amani ziwe juu yake- ndiyo haki, na yasiyokuwa hayo ni upotovu na batili.