U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Suuradda 4

An-Nisaa

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 141

ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓا۟ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَـٰفِرِينَ نَصِيبٌ قَالُوٓا۟ أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ۚ فَٱللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۗ وَلَن يَجْعَلَ ٱللَّهُ لِلْكَـٰفِرِينَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا 141

{141} Kisha akataja uthibitisho wa urafiki wandani wa wanafiki kwa makafiri na uadui wao kwa Waumini, kwa hivyo akasema: "Wale ambao wanawangoja." Yani wanangoja ile hali ambayo mtakayokuwa kwayo, na mtakayoiishia ya heri au ya shari. Wamekwisha itayarishia kila hali jawabu kulingana na unafiki wao. "Basi mkipata ushindi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: kwani hatukuwa pamoja nanyi?" Kwa hivyo, wanadhihirisha kwamba wako pamoja na Waumini kwa dhahiri na ndani, ili wasalimike kutokana na kashfa na shutuma. Na ili washiriki pamoja nao katika ngawira na Fayi (mali iliyopatikana bila ya vita kuwepo), na ili wapate ushindi kupitia kwao. "Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda," na Hakusema Fat-h, (yaani ushindi) wa kuendelea. Kwa sababu hawatakuwa na ushindi ambao ni chanzo cha ushindi wao wa kuendelea. Bali kikomo cha inavyowezafikia ni wao kuwa na sehemu (ya ushindi) isiyokuwa imara, kwa sababu ya hekima kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi Iikiwa hilo, "wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kuwashinda." Yaani, hatukuwa na mamlaka juu yenu, "na tukawakinga na hawa Waumini." Yaani, wanajifanya kuwa walikuwa na uwezo wa kuizuia mikono yao dhidi yao, na kuwazuia kwao na Waumini kwa kila namna ya kuwazuia kama vile kuwapoteza, na kuwavunja moyo dhidi ya kupigana vita, na kuungana na maadui dhidi yao, na mengineyo katika yale yanayojulikana kutoka kwao. "Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Qiyama," na awalipe Pepo wale wanaoamini kwa dhahiri na kwa ndani, na awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake. "Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini." Yaani, kwa kuwapa mamlaka, na utawala juu yao. Bali halitaacha kundi katika Waumini kuwa na ushindi kwenye haki, hatawadhuru mwenye kuwaangusha wala mwenye kuwahalifu. Na hataacha Mwenyezi Mungu kuwafanyia Waumini miongoni mwa sababu za ushindi na kuzuia mamlaka ya makafiri , jambo ambalo linashuhudiwa kwa macho, hadi baadhi ya Waislamu ambao wanatawaliwa na makundi ya kikafiri wamebaki wameheshimiwa bila ya wao kugusa dini zao na wala hawawi duni kwao. Bali wana utukufu kamili kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Basi ni za Mwenyezi Mungu sifa njema zote kwanzo na mwisho, kwa dhahiri na kwa ndani.