Az-Zumar
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
بَلِ ٱللَّهَ فَٱعْبُدْ وَكُن مِّنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ 66
{66} Kisha akasema: "Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu." Aliposema kuwa watu wajinga wanamuamrisha Mtume kufanya ushirikina, na akaeleza ubaya wake, akamuamrisha akusudiwe Yeye peke yake. Akasema: "Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu." Yaani msujudie Yeye peke yake kwa ibada zako, bila mshirika yeyote, "na uwe miongoni mwa wenye kushukuru" Mwenyezi Mungu kwa kukuwezesha kufanya hivyo. Kwani, kama vile Yeye [Mtukufu] anavyoshukuriwa kwa neema za kidunia kama vile afya ya kimwili, usalama, riziki na mengineyo, pia anashukuriwa na kusifiwa kwa neema za kidini, kama vile kumuwezesha mja kumkusudia Yeye tu na uchamungu. Bali, neema za kidini ndiyo neema halisi. Mtu anapotafakari kwamba zimetoka kwa Mwenyezi Mungu, na kumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, anapata usalama kutokana na ugonjwa wa majivuno ambao unawapata wengi wa watendao matendo kwa sababu ya ujunga wao. Vinginevyo, ikiwa mja angejua uhakika wa hali hiyo, hangejivuna kwa neema ambayo inastahili aongeze kushukuru kwa sababu yake.