Al-Baqara
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِى ٱلْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ ٱلْحَرْثَ وَٱلنَّسْلَ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ ٱلْفَسَادَ 205
“Na akishageuka akaenda,” huyo ambaye kauli yake hukupendeza anapokuwa pamoja nawe; “anazunguka katika ardhi ili afanye humo ufisadi.” Yani anajitahidi kufanya maasia ambayo ni kufanya uharibifu katika ardhi, “na anaharibu” kwa sababu ya hilo “mimea na viumbe”. Kwa hivyo, mimea, matunda na mifugo vinaharibika na vinapunguka na baraka zake zinakuwa chache kwa sababu ya matenddo yake. “Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.” Na kama hapendi ufisadi, basi yeye humchukia mja anayefanya ufisadi katika ardhi kuchukia kukubwa, hata akisema kwa ulimi wake maneno mema. Katika Aya hii, kuna dalili ya kwamba maneno yanayotoka kwa watu siyo ushahidi wa ukweli wala uwongo, wala wema wala upotovu; mpaka yapatikane matendo na yanayoyasadikisha, yenye kuyatakasa, na kwamba ni lazima kupima hali ya mashahidi. Na aliye katika haki na aliye katika batili miongoni mwa watu, kwa kuchunguza matendo yao yote, na kuangalia yale yanayofungamana na hizo hali zao. Na kwamba mtu asidanganyike na kujionyesha kwao na kujitakasa kwao nafsi zao. Kisha akataja kwamba mharibifu huyu katika ardhi kwa kumuasi Mwenyezi Mungu anapoamrishwa kumcha Mwenyezi Mungu, anafanya kiburi na ukaidi.