U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Maryam
Suuradda 19

Maryam

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 10

قَالَ رَبِّ ٱجْعَل لِّىٓ ءَايَةً ۚ قَالَ ءَايَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ ٱلنَّاسَ ثَلَـٰثَ لَيَالٍ سَوِيًّا 10

{10} "Akasema: Mola wangu Mlezi, nijaalie Ishara" ili moyo wangu utulie kwayo, na hii siyo kwa sababu ya kuwa na shaka katika habari za Mwenyezi Mungu. Lakini ni kama vile kipenzi wa Mwenyezi Mungu (Ibrahim), amani iwe juu yake, alivyosema, "Mola wangu Mlezi! Nionyeshe vipi unavyofufua wafu. Mwenyezi Mungu akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! Lakini ili moyo wangu utue." Kwa hivyo, akawa ameomba elimu zaidi na kufikia jicho la yakini baada ya kujua kwa yakini. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamuitikia ombi lake kama rehema kwake. "Akasema Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa usiku tatu, na ilhali u mzima sawasawa." Na katika aya nyingine, "siku tatu, isipokuwa kwa kuashiria tu" na maana yake ni sawa. Kwa sababu wakati mwingine alisema usiku, na wakati mwingine akasema siku. Na hili ni katika ishara za ajabu. Kwa maana, kumzuia kuzungumza kwa muda wa siku tatu na kutoweza kwake kufanya hivyo bila kuwa bubu wala balaa yoyote, bali alikuwa mzima sawasawa bila ya kuwa na upungufu wowote, ni katika ushahidi wa uwezo wa Mwenyezi Mungu wa kimiujiza unaoenda kinyume na ada ya kawaida. Na tena pamoja na hayo alikuwa amezuiwa kuzungumza maneno yanayohusiana na wanadamu na kuwaongelesha. Lakini kumtakasa Mwenyezi Mungu [na kusema kuwa hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu] na dhikri na mfano wake, hayo hakuzuiwa kuyafanya. Na ndiyo maana, akasema katika aya nyingine, "Na mdhukuru Mola wako Mlezi kwa wingi na mtakase jioni na asubuhi."