U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
Suuradda 18

Al-Kahf

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 22

سَيَقُولُونَ ثَلَـٰثَةٌ رَّابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًۢا بِٱلْغَيْبِ ۖ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ ۚ قُل رَّبِّىٓ أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ ۗ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَآءً ظَـٰهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِم مِّنْهُمْ أَحَدًا 22

{22} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu kuhitalifiana kwa Watu wa Kitabu kuhusu idadi ya watu wa Pangoni, tofauti inayotokana na kubahatisha kwao ghaibu na kusema wasiyoyajua. Na kwamba wao wana rai tatu juu yao: Miongoni mwao wapo wanaosema: "Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao", na miongoni mwao wapo wanaosema: "Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao." Na baada ya maneno haya mawili Mwenyezi Mungu akataja kuwa huku ni kubahatisha kwao tu ghaibu, kwa hivyo hilo likaashiria ubatili wake. Na miongoni mwao wapo wanaosema: "Walikuwa saba na wa nane wao ni mbwa wao." Na idadi hii- na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi - ndiyo idadi sahihi. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alibatilisha zile mbili za mwanzo na hakubatilisha hii, kwa hivyo hilo likaashiria usahihi wake. Na huku ni katika kuhitilafiana ambako hakuna manufaa yoyote ndani yake, wala hakuna masilahi yoyote kwa watu ya kidini wala ya kidunia yanayopatikana katika kujua idadi yao. Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema, "Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anayejua sawa sawa hesabu yao. Ni wachache tu wanaowajua.” Na hao ndio wale walioafikiana na usahihi, na wakajua kuwa wamepata usahihi. "Basi usibishane juu yao isipokuwa kwa mabishano ya juu juu tu hivi." Yaani bishana, tu kubishana kulikojengeka juu ya elimu na yakini, na ambako kuna manufaa. Ama kubishana kulikojengeka juu ya ujinga na kubahatisha tu ghaibu au ambako hakuna faida yoyote, ima kwa kuwa mpinzani ni mkaidi, na ima kwa kuwa suala lenyewe halina umuhimu wowote wala hakuna faida yoyote ya kidini inayopatikana kwa kulijua, kama vile idadi ya watu wa Pangoni na kadhalika. Kwa maana, kukithiri katika kuyajadili hayo na kuyafanyia utafiti wa mfululizo ni kupoteza tu muda na kuathiri kusikofaa katika mapenzi ya mioyo. "Wala usiulize habari zao yeyote yule miongoni mwao." Na hayo ni kwa sababu maneno yao juu yao yanatokana na kubahatisha tu ghaibu na kuwa na dhana ambayo haina faida yoyote mbele ya haki. Basi ndani yake kuna ushahidi wa kukataza kumuuliza uamuzi wa kidini yule asiyefaa kutoa uamuzi huo. Ima kwa sababu ya upungufu wake katika jambo hilo linalotafutiwa fatwa, au kwa sababu hajali anayoyasema, na hata hana uungwana wa kumzuia. Na ikiwa imekatazwa kuulizwa fatwa watu wa sampuli hii, basi yeye mwenyewe kukatazwa kutoa fatwa ni bora zaidi na ni jambo linalofaa zaidi. Aya hii pia ina ushahidi kwamba mtu anaweza kukatazwa kuulizwa fatwa katika jambo moja na si lingine. Kwa hivyo anaweza ulizwa fatwa kuhusu jambo ambalo anastahiki, tofauti na lingine asilostahiki. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuwakataza kuwauliza kabisa kabisa, bali alikataza kuwauliza kuhusu kisa cha watu wa pangoni na mambo yanayofanana na hayo.