Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Surah 9

At-Tawba

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 30

وَقَالَتِ ٱلْيَهُودُ عُزَيْرٌ ٱبْنُ ٱللَّهِ وَقَالَتِ ٱلنَّصَـٰرَى ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ ٱللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَٰهِهِمْ ۖ يُضَـٰهِـُٔونَ قَوْلَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَبْلُ ۚ قَـٰتَلَهُمُ ٱللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ 30

{30} Wakati Yeye Mtukufu alipoamrisha kupigana vita na Watu wa Kitabu, akataja katika kauli zao ovu zinazowachochea Waumini ambao wana ghera juu ya Mola wao Mlezi na Dini yao juu ya kupigana vita nao na kufanya bidii na kufanya uwezo wao katika hilo. Kwa hivyo, akasema, "Na Mayahudi walisema: Uzeir ni mwana wa Mwenyezi Mungu." Na maneno haya, hata kama siyo maneno yao wote, lakini kuna kikundi miongoni mwao kilichoyasema. Kwa hivyo, hilo linaonyesha kwamba kuna uovu na shari katika Wayahudi, ambayo yaliwafikisha kusema maneno haya ambayo walifanya ujasiri ndani yake kwa Mwenyezi Mungu na wakapunguza Ukuu wake na Utukufu wake. Na ilisemwa kwamba sababu ya wa kudai kwamba Uzair ni mwana wa Mwenyezi Mungu ni kwamba wakati wafalme walipopewa mamlaka juu ya Wana wa Israili na wakawatenganisha kutenganisha kukubwa, na wakawaua wabebaji wa Torati, wakampata Uzair baada ya hayo hali ya kuwa ameihifadhi yote au nyingi yake. Kwa hivyo akawasemea kuiandika kutoka kwa kuhifadhi kwake, nao wakaiandika katika nakala. Kwa hivyo, wakadai kuhusiana naye madai haya mabaya. Nao Wakristo walisema: Isa mwana wa Mariamu ni "mwana wa Mwenyezi Mungu." Mungu Mwenyezi Mtukufu akasema: "hiyo" kauli ambayo waliisema, "ni kauli yao tu kwa vinywa vyao" hawakuimamishia hoja yoyote wala uthibitisho. Na yeyote ambaye hajali kile anachosema, basi haishangazi kutoka kwake kauli yoyote ile anayoisema. Kwa maana yeye hana dini wala akili inayoweza kumzuia kutokana na kile anachotaka kusema, na ndiyo maana akasema: "Wanayaiga" yaani, wanajifananisha katika kauli yao hii "maneno ya wale waliokufuru kabla yao." Yaani, kauli ya washirikina ambao wanasema kuwa malaika ni mabinti za Mwenyezi Mungu. Nyoyo zao zilifanana, kwa hivyo kauli zao zikafanana katika ubatili. "Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!" Yaani, vipi wanageuzwa kutoka katika haki kugeuzwa kuliko wazi, kubainifu kwenda katika kauli batili iliyo wazi?