At-Tawba
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
خُذْ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ 103
{103} Yeye Mtukufu alimwambia Mtume wake na mwenye kushika nafasi yake, akimwamrisha kufanya yale yatakayowatakasa Waumini, na kutimiza Imani yao, “Chukua sadaka katika mali zao” Nayo ni Zaka ya faradhi. "Uwasafishe na uwatakase kwazo;” yaani, uwasafishe kutokana na madhambi na tabia mbaya "na uwatakase;" yaani, uwakuze na uzidishe tabia zao nzuri na matendo mema, na uzidishe malipo yao ya kidunia na ya kiakhera, na uzidishie mali zao, "na waombee dua.” Yaani waombee Waumini kwa ujumla, na kwa namna maalumu kwa kila mmoja wao wanapokupa Zaka za mali zao. "Hakika kuomba dua kwako ni utulivu kwao.” Yaani, ni tulivu kwa nyoyo zao na furaha kwao. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema” dua yako kusikia kwa kuitikia na kukubali. "Mwenye kujua yote“ katika hali za waja wake na nia zao, na atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake na kwa kiasi cha nia yake. Kwa hivyo, Nabii– Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – alikuwa akifuata amri hii ya Mwenyezi Mungu, na anawaamrisha watoe sadaka, na anawatuma wafanyikazi wake kwenda kuzikusanya na kuzileta. Kwa hivyo, anapomjia mtu yeyote na sadaka yake, anamwombea dua na kumbariki. Na katika Aya hii kuna ushahidi juu ya uwajibu wa Zaka katika mali zote. Na kama ni kwa ajili ya biashara, basi hilo ni dhahiri. Kwa maana, hizo ni mali zinazokuwa na mtu anachuma kwazo. Basi katika uadilifu ni kwamba awafariji masikini kwayo kwa kutoa Zaka ambayo Mwenyezi Mungu amewajibisha ndani yake. Na zisizokuwa mali za biashara, basi ikiwa mali hiyo inakua, kama vile nafaka, matunda, na mifugo inayochukuliwa kwa ajili ya kukuza, na maziwa, na kuzaana, basi Zakat ni wajibu ndani yake; vinginevyo, haiwi wajibu ndani yake. Kwa sababu ikiwa ni kwa ajili yake tu, haitakuwa mali hiyo kama mali ambazo mtu huchukua katika hali ya kawaida kwa ajili ya biashara, na kutafuta kwayo madhumuni ya kibiashara. Na hazikufanywa kuwa za kibiashara kwa sababu ni za matumizi ya kibinafsi na mfano wake. Na ndani yake kuna kwamba, mja hawezi kujisafisha na kujitakasa mpaka atoe Zaka ya mali yake, na kwamba haisamehewi kwa chochote isipokuwa kwa kuitoa. Kwa sababu utakaso na usafishaji hutegemea kuitoa. Na ndani yake pia kuna pendekezo la imamu au mwakilishi wake kumwombea baraka yule aliyetoa Zaka yake, na kwamba hilo linafaa kuwa kwa sauti kubwa ili mtoaji asikie na awe na utulivu juu ya hilo. Na inachukuliwa kutoka katika maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya hii kwamba, inampasa mtu kumfurahisha Muumini kwa maneno laini, na kumwombea dua, na mfano wa hayo miongoni mwa yale ambayo yanampa utulivu kwa moyo wake [na kwamba inapaswa kumtia moyo mwenye kutoa matumizi, na akatenda matendo mema kwa kumwombea dua na kumsifu na mfano wa hayo].